Leo Ninaleta Kwako Neno Sanjari na Maelekezo Machache Kwetu Kanisa[cite: 19]
KUISHI MAISHA YA USHINDI
2 Tim 3:1-15
“Kwa matunda yake mti hutambulikana.”
— Mathayo 12:33
(AICT Makongoro - 18/01/2009)
Kwa tabia za wanadamu na mwenendo wa dunia hii ilivyo sasa, tutambue kuwa kweli hivi sasa tu katika nyakati za mwisho Nyakati zinazoonyeshwa matunda yake na 2 Tim 3:1-9 2 Tim 3:10-17 ni mwitikio wetu unavyotakiwa kuwa Mwitikio utakaotuwezesha kuishi maisha ya ushindi Sasa hivi tusimame imara dhidi ya hali halisi tunayokabiliana nayo, hatunabudi tuyajue mambo haya yafuatayo Mambo ambayo kwa upande mwingine yatatusaidia katika kazi zetu za kila siku mwaka huu na kuishi kwa ushindi
1. Ili tuwe na maisha ya ushindi mwaka huu, jambo la kwanza ni kujua mashambulizi ya Shetani yalivyo
- (i) Hushambulia baadhi ya vyuo vya Biblia na seminari mahali walimu na wanafunzi wanadai kuijua Biblia kuliko inavyofundisha Akiinua wahubiri wenye lengo la kufurahisha watu kuliko kusema nini Mungu anataka wasikie
- (ii) Anainua manabii na walimu wa uongo wenye mvuto wa kusikilizwa na watu Jim Murphy anasema nakuu, “Shetani amewawezesha wengi wa watu hao kifedha katika huduma zao ili kuwapotosha wengi”
- (iii) Si hivyo tu bali analishambulia kila kanisa lililo la kibiblia akieneza uzushi na uongo dhidi ya Wakristo wenye ushuhuda safi Kana kwamba hiyo haitoshi, anawashambulia watumishi wa Mungu kutoka ndani na nje ya kanisa ili ikiwezekana wakate tamaa na wawatumaini wanadamu, wawe na kigugumizi katika kukemea maovu
- (iv) Ameamua kulidhoofisha kanisa kwa kuweka vipingamizi vingi juu ya mafundisho ya Neno la Mungu kwa watoto wetu, lengo lake ni kuona watoto hawalielewi Neno la Mungu ipasvyo Tuweni macho na hila za shetani
- (v) Kusababisha lawama na wakristo kuvunjwa mioyo Watu wanafikia hatua hata ya kughairi kutoa huduma kanisani kwa tafsiri kwamba, nguvu zao, fedha na juhudi zao wanazoweka kanisani hazina maana kama hali ya kiroho ndivyo hivi inavyoonekana
- (vi) Shetani ameamua kuharibu moyo wa maombi kwa Wakristo maana anajua mashambulizi yaliyo makali ni maombi ya Wakristo Tena anajua Wakristo wakiomba watabarikiwa kanisani na Mungu wanaye muomba kanisani Anajua kadri tunavyotumia vibaya muda wetu, ndivyo nguvu za kufanya kazi ya Mungu zinavyozidi kupungua
- (viii) Ameweka moyo mgumu kwa Wakristo ili wasione uwepo wa nguvu za shetani kusudi hatimaye awaangamize milele
- (ix) Analidhoofisha kanisa kwa njia ya kueneza ubinafsi kiasi cha watu kutokuona hatia mioyoni mwao badala yake kuekeleza kila chanzo cha tatizo kwa wengine Tabia hii ilianzia kwa Adamu na Eva, mtu kusukuma tatizo kwa mwingine
- (x) Moyo wa toba umeharibiwa sana na shetani maishani mwa Wakristo
2. Tutambue Mamlaka Yetu
Kwa mfano, Petro na Yohana katika Matendo ya Mitume 3:6 “Kwa Jina la Yesu wa Nazareti, simama uende”, twasoma watu wote walimwona kiwete akienda, akimsifu Mungu (mst 9) Aidha wanafunzi 70 wa Yesu Kristo walishuhudia uwezo wa jina la Yesu katika huduma yao Katika Luka 10:17 twasikia wakisema, “Bwana hata pepo wanatutii kwa Jina lako” Jina la Yesu ni mamlaka pekee tuliyonayo dhidi ya mashambulizi ya adui
3. Jambo la tatu ni kuombea Amani nchini mwetu.
Mtume Paulo aliwafundisha Wakristo wa Korintho namna ya kuomba akisema, “Imekuaje basi? nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia…” 1 Wakorintho 14:15
Ili kanisa tuombe kwa akili hatuna budi kuijua hali halisi ya nchi yetu ilivyo Tuombeni ili suala la OIC na mahakama ya Kadhi, vyombo vilivyo vya kidini viangaliwe kwa hekima kubwa na mamlaka husika Tuliombee Bunge letu lisikose, likaruhusu ufa ukatokea na kusababisha mpasuko mkubwa wa amani nchini mwetu kwa sababu za kidini
Amani ambayo Mungu ametupatia leo yapata miaka 45 ya Muungano wetu Watanzania Watu tunaoheshimu katiba ya nchi inayoruhusu uhuru wa imani na ibada kama tulivyo hivi sasa Tuombeni katika roho lakini pia tuombeni kwa akili ili amani idumu nchini mwetu
4. Kuishi maisha ya ushindi, ni pamoja na kushiriki kwetu katika huduma za maendeleo.
Wajibu wetu kanisa kibiblia ni kumhudumia mwanadamu kikamilifu yaani kiroho, kimwili na kiakili Kila mkristo anatakiwa kujiona kuwa ni mdau wa maendeleo kanisani na katika jamii Pasiwe na mmoja wetu wakusubiri mtu fulani alete muujiza wa maendeleo bali kila mtu asimame katika zamu yake aliyojipanga kuleta maendeleo katika jamii
(cf) Nilizishirikisha baadhi ya kwaya kwamba zikiungama zinaweza zikafanya mradi mkubwa ajabu Kama mradi wa kuwa na kituo cha radio kwaya zetu zinao uwezo huo AICT Chang’ombe wanamradi huu na unaendelea vizuri sana kwa hatua ya studio ya kisasa Kanisa hili limeamua kuanzisha mchakato wa kukusanya fedha za kujenga High School, hatua hiyo ni ya kupongezwa Wote tukiwa wadau, tufahamu hatimaye tutafanikiwa tu
Tuacheni kupoteza muda tukilaumiana tu na kutafuta nani katuangusha Hatutafika popote tukiendelea na roho hiyo Kanisa lililobarikiwa halipaswi kuongozwa na madhaifu yao ya nyuma bali linatatua na kupiga hatua mbele Mwaka huu tutaishi maisha ya ushindi kimaendeleo, tukishiriki kila mtu katika huduma za maendeleo
5. Jambo la tano na la msingi ni Kuwa na Mpango Mkakati.
Sote tumashahidi kwamba mipango ama shughuli nyingi, tena zilizo nzuri tumeshindwa kuzikamilisha Moja ya sababu ni kutokana na kukosekana kwa mpango mkakati Kama kawaida mpango mkakati hutumika kama dira ituelekezayo kufikia ono letu vizuri Bila kuwa na dira hii, huwa ni vigumu sana hata kuwajibishana, maana shughuli zetu zitakuwa hazijaratibiwa nani atekeleze nini na lini
Hii ndiyo sababu tuna kazi nyingi zilizokomea njiani baada ya kuanza vizuri Mtu mmoja alisema kweli kwamba wewe usipokuwa na mpango mkakati atakuja mwingine aliye na mpango wake na atakushawishi utekeleze mpango wake
Mwaka huu na maishani mwetu tukimbieni mbio zetu siyo mbio za wengine na tuzikamilishe Hatari ya kuanzisha mambo mengi kwa mara moja yasiyothibitiwa na mpango mkakati, matokeo yake ni kushindwa kukamilisha hata moja ya yaliyoanzishwa
Kwa nini hutokea hivyo?
Hii hutokana na dhana mbaya inayojengeka akilini mwa watu kwamba, iwapo kazi iliyoanzishwa kwanza haijakamilika, itawezekanaje hii mpya ikamilike?[cite: 19] Maana mikono iliyoshindwa kukamilisha kazi ile ya kwanza ni ile ile inayoanzisha kazi mpya Siri kuu ya kufanikiwa katika shughuli na huduma zetu ni pale tunapokuwa na mpango mkakati
Niombe “local church” hii ama pastorate kwa ujumla wake ijiwekee mpango mkakati utakaoratibu shughuli za 2009 na hata kipindi cha miaka 5 ijayo Acha nidiriki kuwaambia kuwa pastorate hii uwezo huo inao
6. Ushindi wetu aidha utachochewa na ujuzi wetu mzuri juu ya nyakati.
Mwaka jana makanisa mengi kipastoreti yalipata nafasi ya kuwa na semina juu ya mada hii inayohusu namna ya kuzijua nyakati Nyakati zilizobuniwa na Mungu mwenyewe na kuelezwa kwa njia ya mfano tuusomao katika Mathayo 20:1-16 Katika mfano huo tunaona watumishi walioajiriwa jioni saa 11, saa ile ya mwisho Kwa tafsiri za kitheologia na kimisioni, watumishi hao ndio sisi Wakristo wa karne hii ya 21 na kuendelea hadi Yesu atakaporudi
Watumishi wenye sifa mahususi za:
- (i) Ubunifu kazini[cite: 19]
- (ii) Siyo tegemezi bali wajasiriamali wazuri[cite: 19]
- (iii) Wavumilivu[cite: 19]
- (iv) Wenye kujitolea na kujituma[cite: 19]
Mfano ni sisi viongozi wa nyakati hizi, tuliopewa neema ya kutosha kuvumilia mishale na mawe yanaporushwa kwetu, utadhani tumewekewa gamba mwilini lisiloruhusu maumivu kupenya ndani Kwa nini? Kwa sababu tunajua wakati huu ni wa mwisho uliotabiriwa kwamba utaghubikwa na uasi mkubwa haijawahi kutokea
Hata hivyo Biblia yatoa onyo kali kwao wote wanaotekeleza unabii wa kutenda maovu kwamba mwisho wao utakuwa dhahiri 2 Tim 3:8-9 “…watu hao walioharibikiwa akili zao walipingana na ile kweli wamekataliwa kwa mambo ya imani, upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama vile upumbavu wa Yane na Yambre ulivyokuwa dhahiri.”[cite: 19]
Wapendwa, tukizijua vizuri nyakati, hasa wakati wetu huu wa saa ya mwisho tutasimama imara katika neno la Mungu na pia tutegemee kubarikiwa na Mungu Sasa ili mtu ubarikiwe mpende hata mtu anayejiita adui wako Ili kanisa hili libarikiwe na Mungu tudumisheni moyo wa upendo siyo masengenyo na mbegu za fitina Tutashangaa tutakaposhuhudia baraka za Mungu Hata mambo yaliyoonekana magumu yatalainishwa na mazingira ya upendo na amani
7. Kufanikiwa kwetu pia kutachochewa na jambo la saba, Uwazi kanisani.
Uzushi na uongo mwingi uwezao kusikika kanisani sehemu kubwa hutokana na ukosefu wa uwazi Dayosisi imo mbioni kutoa chapisho litakalowahabarisha wakristo kila mara juu ya nini kinachoendelea ndani ya dayosisi yetu Najua chombo hiki hakitakuwa ndiyo utatuzi wa uzushi na uongo bali kila kiongozi atatakiwa atoe taarifa sahihi na kwa wakati unaotakiwa ili kuepusha tafsiri zisizo sahihi kutolewa na walio wepesi kusema
(cf. watu wenye michango mdomoni ni wepesi kusema lolote kwa mtindo wowote)
Kamwe tusiwachokoze watu kwa kuwanyima haki yao ya kupokea habari zinazohusu taasisi yao na jamii inayowazunguka Mtu atakayefanya kinyume cha hili, atakuwa ameamua kumsaidia shetani kulijeruhi kanisa la Kristo Isiwe hivyo![cite: 19]
8. Mwisho nitaje tu mambo tunayotakiwa kuwa watekelezaji.
- (i) Maamuzi na maelekezo hutoka mabaraza yaliyo juu yetu, tuyaheshimu
- (ii) Pastoreti zilishaelekezwa kuboresha usafiri wa watumishi[cite: 19]
(mf: Pikipiki ama gari kama vile Bulima Nassa Baiskeli 10, pikipiki na Mei 2009 wana lengo la gari la mchungaji. Tarehe 28/09/2009 nilizindua)
- (iii) Tusimamie vizuri utume wetu wa kumhudumia mwanadamu kiroho, kimwili, kiuchumi na kielimu
Tunamshukuru Mungu dayosisi itakuwa na High School Kijima kuanzia March 2009, itakayoanza kwa hatua za form 1 na baadae kuendelea form V
- (iv) Tushiriki kikamilifu katika maandalizi na maadhimisho yenyewe ya miaka 100 ya kanisa letu
Viongozi nawasihi muwataarifu watu kila kipengele kinachomtaja mshirika wao Tusimame kama washindi tukikataa kuteswa na adui wetu shetani na kumpa tamko kwa kutumia mamlaka tuliyopewa sisi watoto wa Mungu
- Tukatae mashambulizi ya shetani[cite: 19]
- Tutambue mamlaka yetu[cite: 19]
- Tuombee Amani[cite: 19]
- Tushiriki katika maendeleo[cite: 19]
- Tuwe na Mpango mkakati[cite: 19]
- Tukizijua vizuri nyakati[cite: 19]
- Tukichochea uwazi kanisani na kuwa[cite: 19]
- Waekelezaji wa yale tunayokubaliana[cite: 19]
TAMKO
Shetani, falme, mamlaka na jeshi la pepo; ninawatangazia kwamba siku hii ya leo, watu wa familia yangu na mimi mwenyewe, hamna nguvu tena wala mamlaka ya kuwadhuru au kuwagusa kwa namna yoyote ile Mtakaa mbali na nafsi zetu, fedha zetu, mali na kila kitu tulicho nacho Ninatoa tamko hili kwa mamlaka niliyonayo ambayo nimepewa na Yesu Kristo
Baada ya tamko kama hili, likitoka nafsini, amini utasimama na kuishi maisha ya ushindi na Jina la Bwana kutukuzwa ndani yako Amina
Bwana akubarikie na kukulinda Bwana akuangazie nuru za uso wake na kukufadhili na akuinulie uso wake na kukupa amani katika Jina la Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, Amina
